Machapisho

MAPEMA TU KAZI ISHAISHA TAIFA, MIFUMO NA MBINU ZA MAKOCHA WOTE WA YANGA NA AZAM FC NI PACHA

Picha
MAPEMA TU KAZI ISHAISHA TAIFA, MIFUMO NA MBINU ZA MAKOCHA WOTE WA YANGA NA AZAM FC NI PACHA.  ITAFAHAMIKA leo baada ya dakika 90 zile tambo za Yanga na Azam FC ambazo zilikuwa zinatawala kwa kila mmoja kuvuta kwake Uwanja wa Taifa. Mashabiki watakuwa wameshatambua nani atakuwa mbabe leo ataongeza hatua mbele hasa ukizingatia kwamba vita ya nafasi kwa sasa ni kubwa. Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael raia wa Ubelgiji ikiwa nafasi ya tatu na pointi 55 itamenyana na Azam FC iliyo chini ya Mromania, Aristica Cioaba iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 zote zimecheza mechi 29. Mbinu za Mbelgiji wa Yanga Kocha Eymael kwenye mazoezi yake ya hivi karibuni amekuwa akiwanoa wachezaji wake kufunga mabao ya ndani ya 18 ili kupata ushindi.  Eymael ameliambia Spoti Xtra kuwa ana matumaini wachezaji wake wataingia uwanjani wakiwa na hesabu za kulipa kisasi. “Nina amini utakuwa ni mchezo mzuri na wachezaji wangu wataingia uwanjani wakiwa na hesabu za kulipa kisasi ukizingatia kwamba kwenye

MATOKEO YA MECHI ZOTE NDANI YA LIGI KUU BARA

Picha
 Coastal Union 0-0 Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.  Mbeya City 0-1 Alliance, (Juma Nyangi 19’) Uwanja wa Sokoine.  Ndanda SC 1-0 Biashara United (Abdul Hamisi 90’+3 p), Uwanja wa Nangwanda Sijaona.  JKT Tanzania 2-0 Singida United (Musa Said 11’, Hafidh Mussa 61’), Uwanja wa Jamhuri. Simba 3-0 Mwadui FC (Dilunga 9’, Austino 21’ OG, John Bocco 58’), Uwanja wa Taifa.  Namungo FC 2-0 Kagera Sugar (Hashim Manyanya 14’, Reliants Lusajo 77’), Uwanja wa Majaliwa.  Polisi Tanzania 1-1 Lipuli FC (Baraka Majogoro 50’ | Rashid Hassan 63’), Uwana wa Ushirika, Moshi.  KMC 2-1 Ruvu Shooting (Charles Iranfya 29', Emmanuel Mvuyekure 65’ | Graham Naftal 53’), Uwanja wa Uhuru.

SIMBA SC KUMPA KICHAPO MWADUI FC

Picha
FT:Simba 3-0 Mwadui FC Uwanja wa Taifa Dakika ya 71 Mlipili anaingia anachukua nafasi ya Kapombe Dakika ya 67 Malika anaingia kuchukua nafasi ya Raphael wa Mwadui Dakika ya 62, Kagere anaingia anatoka Bocco, Chama anaingia Luis, Kahata ameingia nafasi ya Dilunga Dakika ya 57 Goooal Bocco kwa kichwa Dakika ya 55, Tshabalala anakosa nafasi ya wazi ndani ya 18 Dakika ya 50 Mdamu anafanya jaribio akiwa nje ya 18 linapaa mazima Dakika ya 48 Kened Juma wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Raphael Kipindi cha pili kimeanza HT: Simba 2:0 Mwadui FC Dakika 2 zinaongezwa Dakika 45 zinakamilika Uwanja wa Taifa Dakika ya 44 Mfaume anafanya jaribio linaishia mikononi mwa Manula Dakika ya 43 Mwadui wanalifuata lango la Simba Dakika ya 41 Luis anaotea akiwa ndani ya 18 Dakika 40 Ndemla anamtafuta Dilunga Dakika ya 38 Dilunga anampenyezea Bocco mpira unaokolewa Dakika ya 36 Mwadui wanamiliki mpira, wanapata kona inaokolewa na Manula Dakika ya 34 Luis anapaisha moira akiwa ndani ya 18 D