MAPEMA TU KAZI ISHAISHA TAIFA, MIFUMO NA MBINU ZA MAKOCHA WOTE WA YANGA NA AZAM FC NI PACHA
MAPEMA TU KAZI ISHAISHA TAIFA, MIFUMO NA MBINU ZA MAKOCHA WOTE WA YANGA NA AZAM FC NI PACHA. ITAFAHAMIKA leo baada ya dakika 90 zile tambo za Yanga na Azam FC ambazo zilikuwa zinatawala kwa kila mmoja kuvuta kwake Uwanja wa Taifa. Mashabiki watakuwa wameshatambua nani atakuwa mbabe leo ataongeza hatua mbele hasa ukizingatia kwamba vita ya nafasi kwa sasa ni kubwa. Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael raia wa Ubelgiji ikiwa nafasi ya tatu na pointi 55 itamenyana na Azam FC iliyo chini ya Mromania, Aristica Cioaba iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 zote zimecheza mechi 29. Mbinu za Mbelgiji wa Yanga Kocha Eymael kwenye mazoezi yake ya hivi karibuni amekuwa akiwanoa wachezaji wake kufunga mabao ya ndani ya 18 ili kupata ushindi. Eymael ameliambia Spoti Xtra kuwa ana matumaini wachezaji wake wataingia uwanjani wakiwa na hesabu za kulipa kisasi. “Nina amini utakuwa ni mchezo mzuri na wachezaji wangu wataingia uwanjani wakiwa na hesabu za kulipa kisasi ukizingatia kwam...